BAADA ya kusumbuliwa na presha ya kushuka mara kwa mara, iliyosababishwa na stress za kutendwa na wanaume, hatimaye msanii wa filamu Bongo, Tamrina Poshi ‘Amanda’ ametuliza mzuka baada ya kumpata mpenzi mpya anayeishi ughaibuni.
Akipiga stori na gazeti hili majuzi, Amanda alisema ni kweli kwa sasa ana furaha baada ya kumpata mwanaume anayeamini ni muaminifu baada ya watu wake wa zamani kumtenda na hivyo kujikuta akiwa katika hali mbaya.
“Kwa kweli hivi sasa nipo poa sana. Mpenzi wangu anaishi Europe na siwezi kumtaja jina wala uraia wake kwa sasa, kwa sababu naogopa kuibiwa, pia nataka nifanye sapraizi kwa mashabiki na marafiki zangu, siku ikifika ya utambulisho watamuona,”alisema.