MWANADADA anayefanya vizuri katika muziki Bongo, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’ kwa sasa amejiweka kimapenzi na msanii anayetamba Kenya, Kevin Wyre baada ya kuwepo kwa tetesi za kutemana na mtu wake wa awali, Joe Kairuki aliyekuwa pia ni meneja wake.
Mwanadada anayefanya vizuri katika muziki Bongo, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’ akipozi na Kevin Wyre.
Watu walio karibu na wawili hao wanasema uhusiano huo unafanywa kwa siri ili usivuje na kwamba kwa sasa pia wanafanya kazi ya pamoja itakayokuwa hewani wakati wowote muda mfupi ujao.