Baiskeli ya walemavu iliyotolewa na msamalia mwema wa Maryland Marekani, Joyce Rwehumbiza kwenda kwa Bibi Scholastica Mhagama mkazi wa Kijiji cha Lundusi Kata ya Peramiho wilayani Songea Mkoa wa Ruvuma.
MSAMARIA mwema mmoja ametoa baiskeli ya walemavu kwa Bibi Scholastica Mhagama (76) mwenye ulemavu wa miguu aliyeamua kijitengenea jeneza lake atakapozikwa baada ya kuishi maisha ya dhiki na kunyanyaswa bila msaada kutoka kwa jamii anayoishi.
Bibi huyo mkazi wa Kijiji cha Lundusi, Kata ya Peramiho wilayani Songea Mkoa wa Ruvuma anaishi peke yake katika kibanda kilichoezekwa kwa nyasi.
Msamalia huyu kutoka Maryland, Marekani anaitwa Joyce Rwehumbiza na aliguswa na stori.
Joyce Rwehumbiza ameishatuma baiskeli hiyo na inafika Dar es Salaam leo Ahamisi ya Septamba 11, 2014.