Friday, September 12, 2014

HUU NDIO UJUMBE WA LULU MICHAEL KWENDA KWA MAMA YAKE MZAZI, DAH UNAHUDHUNISHA SANA!

STAA wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael 'Lulu' amemfagilia mama yake mzazi Lucresia Karugila kwa kupitia akaunti yake ya Instagram. 
Lulu akiwa katika pozi na mama yake.
Staa huyo ameachia picha yake wakati akiwa mdogo pamoja na mama yake kisha kuandika ujumbe wa kumfagilia mama huyo ambao ulisomeka hivi: 
Ni miaka 19 sasa tangu tulipoanza rasmi mahusiano haya, ni mahusiano ambayo yamekuwa na changamoto nyingi zaidi kwako kuliko kwangu.
Ni mahusiano yanayomiliki mapenzi ya kweli na mapenzi yasiyo na usaliti.
Haijalishi ni mara ngapi niliwahi kukukwaza na kukuumiza lakini hujawahi kuniacha katika hali yoyote na kusema utafute mwingine wa kuwa naye.
Haijalishi ni wangapi wazuri umewahi kuwaona duniani lakini siku zote mimi ni mzuri zaidi katika macho yako.
Haijalishi ni mabaya mangapi unayajua kuhusu mimi lakini unanitunzia siri zote zilizo mbaya na nzuri....wewe ni mtu pekee ninayeweza kusimama duniani na kujivunia kuwa ni wangu peke yangu, unayenipenda kiukweli, huwezi kunisaliti wala kumuona yeyote mwingine bora zaidi yangu hata kama ikiwa kweli..!
Nakuombea afya, furaha, nguvu na siku nyingi za kuishi duniani...! NAKUPENDA MAMA! 
Picha aliyoweka Lulu Instagram akiwa na mama yake enzi hizo.