Tuesday, September 2, 2014

FBI NA APPLE WATOA TAMKO KUHUSU PICHA ZA UTUPU ZA WATU MAARUFU ZILIZOVUJISHWA MTANDAONI

Kitengo maalum cha upelelezi cha Marekani FBI, na kampuni ya Apple wametoa tamko baada ya kuvujushwa kwa picha za utupu za wasanii maarufu wa kike akiwemo muigizaji maarufu Jennifer Lawrence, Kate Upton na Mary Elizabeth Winstead.
Katika tamko la FBI liliripotiwa na NBC News, wameeleza kuwa walikuwa wanafahamu kuhusu vitendo vya wezi wa njia za mtandao kuhack mafaili ya watu maarufu waliyoyatunza kwenye simu zao kwa application za kutunza mafaili mtandaoni na kwamba wameanza kufanya uchunguzi.
“The FBI is aware of the allegations concerning computer intrusions and the unlawful release of material involving high profile individuals and is addressing the matter.” Inaeleza sehemu ya tamko hilo.
Nae msemaji wa Apple anaehusika na applications za kutunza mafaili online ameeleza kuwa kampuni hiyo imeanza pia kufanya upelelezi juu ya tukio hilo.
“We take user privacy very seriously and are actively investigating this report.”