Hamisa Hassani Mobeto amezaliwa mwaka 1994 mkoani Mwanza na kabila lake ni Mnyamwezi. Mwanzo wake katika tasnia ya u-miss na modelling ilianza baada ya hamisa kuibuka mshindi wa shindano la Miss XXL BACK TO SCHOOL BASH Mwaka 2010 iliyoandaliwa na kipindi cha XXL kutoka Clouds Fm. Mwaka 2011 Hamisa alishiriki mashindano ya Miss Dar Indian Ocean na alifanikiwa kushika nafasi ya pili , pia mwaka huohuo alikua mshindi wa pili wa miss kinondoni na kufanikiwa kuingia kwenye Nusu fainali ya miss Tanzania.
Mwaka 2012 hamisa alishiriki kwenye mashindano ya Miss Univeristy Afrika na kuingia hatua ya 10 bora.
Kutokea Hapo hamisa amekuwa gumzo kwenye tasnia ya uanamitindo na filamu pia. Pia amisa ni video vixen na wengi mnaweza kumuona kwenye video ya Quick Rocka ya My Baby. Mwaka 2014 Hamisa alitokea kwenye cover page la Pulse Magazine la Nchini Kenya.
Akiwa Ndio kwanza ana miaka 21 Hamisa ni mtu wa kuangaliwa sana sababu anategemewa kufanya mambo makubwa zaidi.