Mwanadada kutoka kiwanda cha filamu Bongo, Miriamu Jolwa ‘Jini Kabula’ amewaacha watu midomo wazi baada ya kutinga kivazi kilichomuacha wazi mwili wake.
Jini Kabula alitinga kivazi hicho kwenye bethidei ya mtoto wa mwigizaji mwenzake, Riyama Ally ambayo aliiunganisha na ya kwake na kufanya bonge la sherehe katika Ukumbi wa Chamuruma uliopo Mabibo jijini Dar, ambapo mwanadada huyo bila kujali macho ya watu alitinga blauzi nyepesi inayoonesha maungo yake ya ndani yalivyo hivyo kuzua minong’ono kwa baadhi ya waalikwa.
Mwanahabari wetu alipomfuata Jini Kabula na kumuuliza kulikoni kuvaa hivyo alisema haoni shida.