Thursday, September 11, 2014

MAN UTD WASALIMU AMRI WATHIBITISHA UMUHIMU WA DAVID MOYES KLABUNI HAPO

Man Utd Wathibitisha umuhimu wa David Moyes Uongozi wa klabu ya Man Utd umeripoti kupata hasara kubwa ya kipato chake cha kila mwaka licha ya kuonesha faida nzuri wakati wa uongozi wa David Moyes kama maneja.
Taarifa iliyotolewa na uongozi wa klabu hiyo ya nchini Uingereza, imeeleza kuwa kipato chake cha kila mwaka kilishuka kwa asilimia 84, ilihali faida yake iliongezeka kwa zaidi ya asilimia ishirini.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa, uongozi wa klabu hiyo yenye maskani yake mjini Manchester unatarajia kipato chake cha mwaka 2015 kushuka zaidi, kutokana na matokeo mabovu yanayoendelea kuwaandama, hasa kwenye michuano ya ligi kuu ya soka nchini Uingereza, ambapo hatua hiyo inajitokeza kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 20.
Aidha, taarifa hiyo imeonyesha wazi kwamba, wakati wa meneja David Moyes na jopo lake walipata jumla ya Dola milioni nane kama malipo ya kuachishwa kazi mapema mwaka huu baada ya kufanya kazi kwa kipindi cha miezi zaidi ya sita.