Maandamano ya CHADEMA Mkoa wa Dodoma yamedhibitiwa kwa Mkoa mzima.
1. LAURENT S/O MANGWESHI mwenye miaka 36, Mkristo, Msukuma Mkulima wa Wialya ya Mpanda Mkoa wa Katavi.
2. AGNES D/O STEPHANO mwenye miaka 26, Mhehe, Mkristo Mfanyabiashara Mkazi Ubungo MAziwa Dar es Salaam.
3. ELISHA S/O DAUDI mwenye miaka 49, Msukuma, Mkristo Fundi umeme Mkazi wa TAbora.
Kamanda LUKULA – ACP amesema gari hilo lilikuwa na bango lenye maandishi “TUNAPINGA UFISADI UNAOFANYWA NA BUNGE LA KATIBA”. Likiwa na maandishi ubavuni mbele na nyuma M4C.
Aidha Kamanda LUKULA – ACP ameongeza kuwa kabla ya kukamatwa kwa gari hilo Polisi walilikimbiza na katika kupita kwenye kona/mtaa watu wawili waliruka kutoka kwenye gari hilo na kukimbia kusikojulikana na bango hilo. Watu waliobaki ndani ya gari hilo ambao ni wanne ndio waliokamatwa.