Staa wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel amelazimika kusitisha bata alizokuwa akila nchini Marekani baada ya kupata msiba wa mdogo wake aliyefariki dunia juzikati.
Chanzo chetu makini kilieleza kuwa, Aunt alipata taarifa za mdogo wake huyo (si wa damu) aliyekuwa akiishi naye aitwaye Ziada kufariki dunia akiwa mamtoni hivyo ikamlazimu kurudi Bongo ili kushiriki kwenye mazishi.
Ijumaa lilipata bahati ya kuwasiliana na Aunt ambaye alisema ameshitushwa na taarifa hizo na alikuwa njiani kurejea Dar.“Nimeumia sana, Ziada alikuwa ni mdogo wangu tuliyependana sana lakini Mungu kamuita, hakuna jinsi,” alisema Aunt kwa masikitiko.