Hakuna siri ya wawili duniani! Baada ya staa wa sinema za Kibongo, Riyama Ally kumfichaficha mwanaume aliyezaa naye kwa muda mrefu, hatimaye jamaa huyo amenaswa.
Tukio hilo lililopigwa chabo na ‘mtu wetu’ lilijiri wikiendi iliyopita kwenye Ukumbi wa Chabruma uliopo Mabibo, Dar ambako kulikuwa na bethidei ya mtoto wa Riyama aitwaye Fatuma aliyetimiza miaka miwili ambapo alifanya sherehe kama harusi huku akiunganisha na bethidei yake iliyokuwa siku moja kabla ambapo mastaa kadhaa walihudhuria.
Bw. Haggy (Baba Fatuma) akikata keki mwanaye.
Muda mfupi baada ya Riyama na mwanaye kuingia ukumbini, waliofuatia kuingia huku wakicheza muziki kwa staili ya Kisambaa walikuwa ni wakwe, yaani baba wa mtoto na mama yake na ndugu wengine waliowasindikiza.
Baada ya kuingia, sherehe ilianza ambapo mshehereshaji ambaye ni msanii wa filamu, MC Kinyata alimwita mbele baba wa mtoto anayejulikana kwa jina moja la Haggy na kuungana na mzazi mwenzake na mtoto wao na hapo zoezi la kukata na kulisha keki likaanza.
Wawili hao walionekana wenye furaha huku wakilishana keki na kukumbatiana kimalovee hali iliyosababisha ukumbi ulipuke kwa vigelegele na baada ya hapo walikuwa pamoja hadi mwisho wa sherehe.