Saturday, October 11, 2014

AFANDE SELE: KATIBA ALIYOKABIDHIWA KIKWETE INA MAKOSA MENGI, HAITODUMU


Rapper na mwanaharakati Seleman Msindi aka Afande Sele amezungumzia makabidhiano ya katiba mpya yaliyofanyika juzi katika viwanja vya Jamhuri Dodoma ambapo spika wa bunge maalum la katiba, Swamwel Sitta alimkabidhi rais Jakaya Kikwete katiba inayopendekezwa.

Afande Sele amempongeza rais Kikwete kwa hatua hiyo lakini akaonya kuwa katiba hiyo ina makosa mengi.
 
“Kwa namna yoyote inabidi tuikubali ingawa kuna mapungufu yanaonekana,” amesema  Afande Sele  na  kuongeza:
 
 “Kilichofanyika ni katiba lazima ipatikane, lakini bahati mbaya ni kwamba ni katiba ambayo imekosa maridhiano. Inatakiwa ili kufanya kitu hata kama wewe ni baba na unataka kufanya kitu lazima upate maridhiano ya familia yako pamoja na watoto wako, ila kwa sababu serikali imetumia pesa nyingi kuanzia kwa Warioba, sasa ni lazima katiba mpya ipatikane hata bila maridhiano.
 
"Katiba hii imepatikana kwa kundi moja. Yaani chama cha mapinduzi kimeichukua katiba hii kama ya kwake na kuyaacha yale ambayo yalipendekezwa kwenye rasimu ya awali ambayo ilipatikana kupitia tume Jaji Wariomba ambayo iliundwa na rais KiKwete.”
 
“Ukiangalia mpaka sasa hivi rais amekabidhiwa katiba lakini haikuwa na maridhiano, unakuta hao hao walioandaa katiba ndio walioichagua mpaka ikapatikana. Mwanasheria mkuu wa Zanzibar kajiudhuru, hivi ana watu wangapi nyuma yake? Mimi naamini hii ni katiba ambayo ingedumu miaka mia moja ili kuokoa hasara kwenye taifa, lakini katiba hii piga uwa haina miaka ishirini mbele, lazima itabadilishwa tena,” 
 
“Katiba hii ina makosa mengi ndani ila imefosiwa kupita kwa sababu ya kundi moja ila kwa upande wa rais Kikwete kwangu mimi siwezi kumlaumu. Nampa hongera sana kwa kuandaa huu mchakato ingawa kumetokea makosa mengi.”