...hawa jamaa nao waligongana, mwendesha pikipiki na mwenye gari katika eneo la tukio na kuanza 'kuzikunja'.
Mtu mmoja ambaye hakuweza kujulikana jina lake mara moja amepigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi na kuporwa mkoba uliyokuwa garini ambao haukujulikana ulikuwa na nini ndani yake. Tukio hilo limetokea leo majira ya mchana maeneo ya Magomeni Mikumi jirani na kwa Sheikh Yahaya jijini Dar es Salaam. Mtu huyo alipigwa risasi tumboni akiwa kwenye gari yake Toyota Mark II (GX 100) yenye namba za usajili T487 AZW. Kwenye gari hiyo, alikuwemo mwanamke mmoja akiwa amekaa kwenye kiti cha mbele cha abiria ambaye hakujeruhiwa.