Tuesday, October 21, 2014

BEN POL: HUWA SIWAACHI WANAWAKE, TUNAACHANA

Makala: SHANI RAMADHANI
NI siku nyingine tena tunapokutana na Benard Paul ‘Ben Pol’ kwenye Live Chumba cha Habari cha Global Publishers, ni mwanamuziki anayefanya vizuri katika soko la muziki wa Bongo Fleva kupitia wimbo wake wa Jikubali.
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Ben Pol akijiandaa kufanya mahojiano na Global TV online.
Katika mahojiano na safu hii huku akirekodiwa na timu nzima ya Global Tv Online, Ben Pol alisema hajawahi kumuacha mpenzi wake bali huwa anaheshimu sana hisia za mtu.
Ifuatayo ni sehemu ya mahojiano ambayo pia yanapatikana pia kupitia tovuti yawww.globaltvtz.com
Mwandishi: Ulianzaje muziki?Ben Pol: Nilianza muziki baada ya kumaliza elimu ya kidato cha sita mwaka 2010 ambapo nilifanya muziki kwa mwaka mmoja. Nikajiunga na Chuo cha IFM kwa mwaka mmoja na sasa hivi nafanya muziki lakini nina ndoto za kurudi tena shule.
Host wa kipindi cha Mtu Kati cha Global TV, Pamela Daffa akifanya mahojiano na Ben Pol (hayupo pichani)
Mwandishi: Kuna mpenzi wako ambaye mlikuwa kwenye uhusiano kwa muda wa miezi 8 halafu mkaja kuachana, ilikuwaje mpaka ukawa unamficha?
Ben Pol:  Sijawahi kumuacha mtu labda inatokea tu tunaachana lakini mimi huwa  naheshimu sana hisia za mtu na ikitokea kama nilikuwa na mtu halafu tukaachana haimaanishi nimemuacha ila tumeachana.
Mwandishi: Kwa nini wasanii huwa mnaonekana ni watu wa kupenda wanawake sana?
Ben Pol:  Mara nyingi wasanii huwa tunaonekana tunawaacha wanawake au tunapenda sana wanawake na hatutulii na mtu mmoja lakini pia hata wao wanavyokuja kwetu huwa na mafikirio yao waliyokuwa wanategemea, wakiingia wakikuta tofauti wanaingia mitini.
Mfanyakazi wa Global, Andrew Carlos (kushoto) akisalimiana na Ben Pol.
Mwandishi: Vipi kuhusiana na wimbo wa Jikubali kwa sababu inadaiwa kuwa umekopi na kupesti, je ni kweli?
Ben Pol: Kiukweli Jikubali haijakopiwa wala haijapestiwa ila imekuwa ‘inspired’ yaani imetokana na ‘inspiration’ au mfano wa kuigwa, mfano kama mtu  ametengeneza gari halafu mtu mwingine akawa ‘inspired’ akatangeneza sheli.Mwandishi: Ulifikiria nini mpaka ukaamua kuimba jikubali?
Ben Pol: Wakati nataka kutunga wimbo wa ‘ku-inspire’ jamii imenibidi kukusanya nyimbo zote zinazosema ‘you can be a champion’ ‘everything is possible’,
Kiongozi wa Kitengo cha IT, Clarence Mulisa (kushoto) akiwa katika pozi na Ben Pol.
unaweza, yaani ndoto zako zinaweza kutimia ukifanya hivi kwa sababu tutake tusitake hamna kitu kitakachoimbwa sasa hivi ambacho hakijawahi kuimbwa na kinachomata ni namna ya uimbaji ndiyo maana kwa kutumia huu wimbo nikasema ngoja nimwambie kijana wa Kitanzania kwamba ‘you can be anything’ kwa kutumia  Watanzania wenzake wenye mafanikio ndiyo maana ukisikiliza wimbo huo kuna Monalisa, Ray, Linah, Diamond, wanasiasa na wengine wengi.
Mwandishi:Una kitu gani kipya ambacho unataka kuwaambia mashabiki?
Ben Pol: Nataka niwaambie mashabiki zangu kuwa kwa sasa nimejikita sana studio na pia nafikiria muda mwingine nikija tena basi nitaanza kutoka na video.