Diamond Platnumz amewabwaga Davido, Awilo Longomba, Willy Paul Msafi (Kenya) na Eddy Kenzo wa Uganda na kushinda kipengele cha ‘mtumbuizaji bora wa Afrika – Best African Entertainer kwenye tuzo za IRAWMA (International Reggae and World Music Awards).
“It always seems impossible until it’s Done!…ningependa kuwataarifu Wadau wangu kwamba #MdogoMdodo ndio nyimbo bora yenye Mahadhi ya Kiafrika na Kijana wenu Diamond ndio M’burudishaji bora wa Mwaka kwenye tunzo hizi za #IRAWMA zilizofanyika nchini Marekani 04|10|2014….. Asanteni sana sana…hakika Umoja ni nguvu, tuhamieni kwenye nyingine sasa,” ameandika msanii huyo kwenye Instagram.