Tuesday, October 28, 2014

HIVI NDIVYO SOKWE HUYU MWENYE MIAKA 40 AMESHEREHEKEA SIKU YA KUZALIWA.

1414066412783_wps_15_Jeff_Moore_23_10_14_ZaireStori kutoka Uingereza nimekutana nayo mtandaoni mtu wangu wa nguvu, na kama ilivyo kawaida yangu, nafanya kushare na wewe kama hivi.
Na stori hii inamhusu sokwe mmoja ambaye amepewa jina la Zaire, ambaye anafugwa katika bustani moja ya wanyama London, Uingereza amesherehekea siku yake ya kuzaliwa ambapo ametimiza miaka 40.
Na kama haitoshi, party yake ilikuwa poa kama ambazo huwa tumezoea kufanya binadamu, ametengenezewa keki ya nguvu katika sherehe hiyo na moja ya mabingwa wa kutengeneza keki za sherehe, Richard Burr.
Unaambiwa sokwe huyu anapendelea vitu kama jelly zisizo na sukari, apples, na karoti hivyo mwandaaji wa keki alijikuta na jukumu la kuhakikisha anamuandalia keki itakayomfurahisha Zaire.
Hizi ni picha za Sokwe huyo akijiachia na keki akisherehekea.
Gorilla
Zai
Zair
Zaire ii
Zairee
Zra