Saturday, October 18, 2014

KAULI YA DIAMOND PLATNUMZ KUHUSU "KUMSAIDIA" ALIKIBA ILI ATOKE TENA KIMZIKI YAWAKERA MASHABIKI...SOMA ZAIDI



Msanii Diamond Platnumz amewakera mashabiki kutokana na kauli aliyoitoa wakati akizungumzia kufanya collabo na msanii mwenzie, Alikiba, na wasanii wengine. Diamond, akizungumza na Diamond 255 ya XXL ya Clouds Fm, alisema kuwa ana nia na kufanya collabo na Ali Kiba, na wasanii wengine Tanzania; kitu ambacho ni kizuri. Kilichowakera mashabiki hao ni jinsi alivyosema. Nukuhu:
Mimi sina tatizo, inategemea ni project gani inategemea ni muziki gani kwasababu nimeshawasaidia watu wengi nimefanya nao macollabo kwanini mtu anavyokuja nifanye nae collabo yeye nikatae, yaani siwezi kukataa.

Mwaka huu kwanza zitatoka nyimbo nyingi za macollabo ambayo wasanii wengi wa Nigeria nimewasaidia nimefanya nao nyimbo, wengi sana.
  

 Kcee nimefanya nae, nimefanya na Mafikizolo, nimefanya na yule Waje, nimefanya na Don Jazzy, nimefanya na Dr Sid, nimesaidia watu wengi sana. Kwahiyo kama naweza kufanya wa huko kwanini nisifanye na mtu wa nyumbani, nikishindwa kufanya na mtu wa nyumbani nitakuwa na roho mbaya, au nitakuwa sitaki kusaidia kwasababu namshukuru mwenyezi Mungu muziki wangu kidogo umefika hatua sio mbaya, so nikifanya na mtu wa nyumbani na yeye namfikisha katika hatua ambayo hajawahi kufika bado, so mi siwezi kumkatalia mtu yeyote
Hiyo kauli ya kwamba akifanya collabo na msanii yoyote wa Tanzania, atakua “anamsaidia” na “kumfikisha katika hatua ambayo hajawahi kufika bado” ndiyo iliyowakera baadhi ya watoa maoni hao.