Saturday, October 18, 2014

MAPICHA:SIMBA NA YANGA KATIKA PICHA LEO, MAHASIMU WAISHIA KUTOANA JASHO PAMOJA TAIFA


Beki wa Yanga SC, Juma Abdul akiwa amemuangukia mshambuliaji wa Simba SC, Emmanuel Okwi katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana

Kiungo wa Yanga SC, Andrey Coutinho akimiliki mpira mbele ya beki wa Simba SC, William Lucian 'Gallas'
Mshambuliaji wa Yanga SC, Genilson Santana 'Jaja' akitafuta mbinu za kuwatoka wachezaji wa Simba SC
Kipa kinda, Peter Manyika (kulia) akipongezwa na kipa wa kwanza wa timu hiyo, Ivo Mapunda baada ya kumaliza dakika 90 za mpamano dhidi ya Yanga SC bila kugungwa
Jaja akijiandaa kupiga mpira mbele ya Gallas
Beki wa Simba SC, Mohamed Hussein Tshabalala akimzuia mshambuliaji wa Yanga SC, Mrisho Ngassa
Kipa Peter Manyika kulia akimsindikiza kiungo wake, Jonas Mkude wakati anatoka nje baada ya kuumia
-BIN ZUBEIRY