Wednesday, October 29, 2014

KUFUATIA DIAMOND KUTUNUKIWA PHD, HIKI NDICHO ALICHOSEMA MWANDISHI HUYU WA STORY ZA FILAMU

image
Nasib Abdul Diamond Plutinumz
Baada ya Tarifa kutoka Idara ya Sanaa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kusema kuwa tarehe 8 Novemba 2014, Kijana Nassib Abdul atatunukiwa Shahada ya Uzamivu(Phd) na Chuo hicho kwa kuthamini mchango wake kwenye jamii kupitia sanaa.(Honorary PhD in Fine &Perfoming Arts).
image
Zagamba Junior
Zagamba Junior mwandishi wa story za filamu ambaye pia ni mwanafunzi katika chuo cha uandishi, leo ameandika katika mitandao ya kijamii kuwa ni bora akaamua kuacha kusoma na badala yake akazane kujitangaza ili apate umaarufu na hatimaye na yeye atatunikiwa PHD kama msanii Diamond.
image
Zagamba akikabidhiwa cheti na Abdul Simba Mkufunzi wa uandishi
image
Sehemu ya maneno aliyoandika Zagamba
Mashabiki wa Diamond wamepokea kwa furaha taarifa hizi na wengine wameanza kurusha vijembe mitandaoni kujibu mapigo ya waliomzomea Diamond kwenye tamasha la Fiesta mwaka huu.
image
Mdau mmoja wa karibu wa Diamond amenukuliwa kwny ukurasa wake wa Facebook akisema “Ningependa kuwakaribisha Wazomeaji woooteee wenye sauti mbaya sana waweze kufika kwenye Viwanja vya UDSM kushuhudia Tukio la Kihistoria kwa Mtoto huyu wa Tandale ambaye ni BIDII NA HESHIMA Vimemfikisha hapa.”
Baada ya kutunukiwa Shahada hiyo Diamond atatambulika rasmi kama DR.NASIBU ABDUL au Pengine DR.DIAMOND PLATNUMZ au ukitaka swaga unaweza sema DR.PLATNUMZ BABY!
image
Diamond Plutinumz
Baadhi ya watu wameonekana kutoridhishwa na maamuzi ya chuo kikuu cha Dar kumtunuku Diamond PhD wakihuzisha na sababu za kisiasa, huku wengine wakinukuliwa wakisema “Ukistaajabu Uprofesa wa JK utaona PhD ya Diamond