Sunday, October 12, 2014

MARIO BALOTELLI AWAAHIDI MABAO LIVERPOOL KULIPA FADHILA ZA BANGO

MSHAMBULIAJI Mario Balotelli amewashukuru mashabiki wa Liverpool kwa sapoti wanayompa na kuwaahidi kucheza vizuri na kufunga mabao.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ameposti kwenye Instagram jana akishukuru kwa mashabiki wa Anfield kuonyesha imani juu yake na kumpa heshima kwa kupeperusha bango la kumtukuza.
Bango hilo liliandikwa kwa lugha ya nyumbani kwao Balotelli, Kitaliano, likiwa na maana 'Sina cha kuthibitisha zaidi ya ujuzi wangu'.
Mario Balotelli amewaahidi mabao mashabiki Liverpool
Balotelli's post on Instagram thanking the fans for the gesture and assuring them his best is yet to come
Balotelli ameposti kwenye Instagram kuwashukuru mashabiki waliopeperusha bango hilo

Na Balotelli amewajibu katika kwa kusema: "Sina cha kuthibitisha zaidi ya ujuzi wangu? Wow asante kwa yeyote aliyefanya hivi. 
"Nafahamu nyote mnatarajia zaidi kutoka kwangu... Mabao zaidi na hususan ujuzi zaidi, lakini nipeni muda na nitaonyesha ukweli,".
Balotelli amekuwa na mwanzo mgumu Liverpool, akifunga bao moja tu katika mechi nane alizocheza kwenye mashindano yote hadi sasa.