Sunday, October 12, 2014

NANI MTANI JEMBE WAFANYAKAZI WA TBL ARUSHA WAJIGAWA SIMBA NA YANGA...KABURU NA BHINDA WE ACHA TU!


Makamu Rais wa timu ya Simba,Geofrey Nyange Kaburu(kushoto) na Mjumbe Kamati Kuu ya timu ya Yanga,Mohamed Binda,wakicheza danadana wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Nani Mtani Jembe kwenye kiwanda cha Bia mkoani Arusha jana.
Mashabiki wa timu ya Simba na Yanga ambao ni wafanyakazi wa kiwanda cha kampuni ya Bia mkoani Arusha wakivuta kamba jana wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Nani Mtani Jembe iliyowakutanisha wafanyakazi wa kiwanda hicho 
Mashabiki wa timu ya Yanga ambao ni wafanyakazi wa kiwanda cha kampuni ya Bia mkoani Arusha wakishangilia baada ya kuwashinda mashabiki wenzao wa Simba  jana wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Nani Mtani Jembe mkoa wa Arusha  iliyowakutanisha wafanyakazi wa kiwanda hicho.
 

Wafanyakazi wa kiwanda cha Bia,Arusha  ambao ni mashabiki wa timu za Simba na Yanga wakicheza mchezo wa Foosball jana kwenye uzinduzi wa kampeni ya Nani Mtani Jembe ilifanyika kwenye kiwanda hicho.