MREMBO Sitti Mtemvu kutoka Temeke ametwaa taji la Miss Tanzania 2014 na kujinyakulia kitita cha milioni 18 usiku wa kuamkia leo katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Nafasi ya mshindi wa pili imekwenda kwa Lilian Kamazima ambaye amejishindia shilingi milioni 6 huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Jihan Dimachk. Dorice Mollel ameshika nafasi ya nne wakati Nasreen Abdul akichukua nafasi ya tano.
Kwa ushindi huo, Sitti atapeperusha bendera ya Tanzania katika mashindano ya Miss World 2015.
Pichani ni Washiriki waliochaguliwa kuingia kwenye hatua ya tano bora katika shindano la Redds Miss Tanzania 2014 linaloendelea hivi sasa ndani ya ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar.
Mmoja wa Washiriki waliongia katika nafasi ya tanno bora shindano la Redds Miss Tanzania 2014 wakijibu maswali mbalimbali.
Msanii wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz akitumbuiza jukwaani akiwa na Vanessa Mdee mbele ya wageni waalikwa (hawapo pichani),waliofika kushuhudia shindano hilo.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi9fw1BXe07flAegJajIjdFImkotNUXRKdmarFpIeJDzX-5ICUoC_qNmPcG-lEzZ8EL2sWmZMeZAj42r-cgsSx7sGCLIVwkHo5FOtT7046QhpNhssyBao-pwvWBoAiRzxOslJwJA247mmaP/s1600/4.jpg?width=640)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjXRPpPKBjchjKSABQJbSVCbmuiuqBY_UqR_c8TsOEor5w1YzCcI_XjPSiOnG91USDDOrzDRjkjBJzySRxqSJB2nKVQ_NZZGul9lPnQXaiTkAMC0DWfEk_HUxHWpMaIVqN2t7rnD1aHLnd8/s1600/1.jpg?width=640)