Friday, October 31, 2014

SABABU 4 ZA MSINGI KWANINI INABIDI UACHE KUANGALIA P*ORN !!!



Kutokana na kuenea kwa p*orn sikuhizi haitakua kitu cha kushangaza kama baadhi ya watu watajikusanya kufanya uchunguzi kuhusiana na madhara yake . kutokana na uchunguzi uliofanywa na website inayoitwa projectknow.com unasema kuna zaidi ya kurasa millioni mia nne na ishirini (420) ambazo ni maalumu kwa ajili ya p*orn. Wanasayansi kutoka chuo cha cambridge university nchini uingereza walifanya utafiti kuhusiana na jinsi akili inavyoitafsiri p*orn na kugundua hamna tofauti na mtu anayetumia madawa ya kulevya. Kuna research nyingi ambazo hatutaweza kuzimaliza lakini tusipoteze wakati, hizi ndio sababu zitakazokufanya ukiwasha laptop yako uende kuangalia video mpya ya ommy dimpoz youtube au kuchat na washkaji facebook na kuacha kuangalia mambo yetu yale :-

1. Kupoteza maana ya kufanya mapenzi. Kwa mtu wa kawaida anayoangalia p*orn ,maana ya kufanya mapenzi kwake inakua ni kuangalia pich au video ya “chombo” ambacho ni mwanamke. Kwa kitendo hiki, mwanaume ni yeye na nanihii yake na mahitaji yake. Mwanaume anapata demu anayemuhitaji papo hapo na demu huyo kufanya kitu chochote mwanaume anachohitaji bila hata ya hitaji la upande wa pili. Unapata demu asiyetaka kitu chochote, ambae hawezi kukukosoa juu ya utendaji wako wa mapenzi, na hataki kitu zaidi ya wewe kumuangaia. Na muda wote unapoangalia p*orn unadhani ni kwasababu una kiasi kikubwa cha testerone au una msukumo mkubwa wa kimapenzi kuzidi wanaume wengine na kufanya kufanya mapenzi peke yako kua kitu kizuri na unachofanya kila saa. Lakini mwisho wa siku inapokuja kwenye demu halisi aliye uchi ambae labda ni mkeo au demu wako unashidwa kupata mzuka na kusababisha uanze kutumia dawa zetu zile za mitishamba au kama una pesa unaanza kutafuta zile za dukani.



2. P*orn inamuonyesha mwanamke kama kifaa flani hivi…

Watu wengi huangalia p*orn na kufikilia kwamba mambo yaliyopo kwenye p*orn ndio inavyokua kwenye uhalisia wa mapenzi na kusababisha mwanamke kufanyiwa vitu vya ajabu na hata wengine hata kuweza kubaka. Hii ndio sababu kubwa maana halisi ya mapenzi imepotea na watu sasa wanafanya kilichopo kwenye ile video waliyoiona . Mapenzi ni kitu cha asili na ndio maana hamna shule ya mapenzi.



3. Unaweza kupata addiction mbaya sana

Kuangalia p*orn ili kuondokana na kuboreka,matatizo au stress kunaweza kutengeneza njia ya adiction. Unapoangalia p*orn ili kuondokana na stress utafurahia sana lakini pale p*
orn inapoisha na furaha kumalizila ndio stress zitazidi na mwisho wa siku utaangalia tena na tena hadi kusababisha addiction.




4. P*orn inaleta viwango vya uzuri ambavyo hakuna mwanamke anaweza kuvifikia…

Mara nyingi wanawake waliopo kwenye p*orn unakuta wanamaumbo ya ukweli na wengi unakuta wamejazia ile mbaya !!! au sio? sasa kama wewe unapenda kuwaangalia wanawake waliojazia kama sijui nini basi ndio utakua unatamani upate mwanamke kama huyo na mwisho wa siku unapomkosa utapata demu wa kawaida na mahusiano ya kimahaba yasiwe kama ulivyotemewa.