Monday, October 6, 2014

WANASINII WA BONGO MUVI KWELI HAMNAZO KABISA ... TAZAMA HAWA WALIVYONASWA WAKISAGA MIRUNGI

Meza ya wasanii wa filamu Gabo na Bond ikiwa na dozi ya kutosha ya mirungi.

WASANII wa filamu nchini, Bond Bin Sinan na Salim Ahmed ‘Gabo’ hivi karibuni walinaswa wakisaga mirungi hadharani bila kujali kadamnasi.Ishu hiyo ilitokea katika Ukumbi wa Dar West,
Tabata Dar kulikokuwa na sherehe ya bethdei ya Wastara Juma ambapo wasanii hao walikuwa wamejaza mirungi kwenye mfuko wa nailoni na kuweka mezani huku wakitafuna kuanzia mwanzo hadi mwisho wa shughuli.
Gabo aking'ata mirungi.
“Duh! Jamani hawa wasanii wanakula mirungi hapa ukumbini ambako kuna watu kibao na wa aina mbalimbali hawaoni kwamba wanavunja sheria za nchi?” alisikika mmoja wa waalikwa.
Wenyewe walipoulizwa kuhusiana na tukio hilo, hawakuwa tayari kujibu lolote zaidi ya kuendelea kutafuna