Msanii wa filamu nchini Irene Uwoya amefunguka leo katika blog hii... na kusema kuwa yeye hajaachana na mumeo wa ndoa na wala msanii Diamond Platnum hajavunja ndoa yao kama ambavyo baadhi ya watu na vyombo vya habari walivyokuwa wakisema.Uwoya ameweka wazi suala hilo baada ya mashabiki wengi kutaka kujua kama ameachana na mumeo ndikumana na ndipo hapo amekanusha kuwa hajawahi kuwa na mahusiano na Diamond Platnum wala Msanii Msami Baby kama ambavyo watu wamekuwa wakijua ni wapenzi bali amesema kuwa yeye na msanii Msami ni marafiki wa karibu na sasa wanafanya filamu ya pamoja.
Gasper Nataly :una mahusiano ya kimapenzi na Msanii Msami >>>Irene Uwoya: hapana Donlee Guck i love my sister,unachukuliaje skendo za wa sanii bongo?,kwanini uliamua kuachana na Mr Ndikumana>>>>>Irene Uwoya kawaida hatujaachana SINA BIFU NA JACKLINE WOLPERKuna wakati uvumi ulienea kuwa Irene Uwoya amekuwa na bifu na msanii mwenzake wa Filamu Jackline Wolper lakini leo kupitia Kikaangoni Live Irene Uwoya amekana kuwa na bifu na Wolper na kudai kuwa Jackline ni mtu wake wa karibu ambae amekuwa akimshirikisha katika mambo mbalimbali hali ambayo anamfanya ajione ni kama pacha wake kutokana na kuelewana na kushabiana katika mambo mbalimbali. Tuma Simba Ni kweli bifu lenu ww na jacline wolper limemaliza?
>>>>>>Irene Uwoya hatuna bifu na pacha wangu Wolper. SIWEZI KUVAA NGUO NDEFU Uwoya ambaye huwa ni hatari sana akiwa katika kazi yake ya uigizaji hususani zile scene za mahaba niuwe amesema kuwa katika maisha yake ya kawaida mbali na uigizaji amekuwa akizichukia na kutozipenda nguo ndefu hiyo ndiyo sababu inayomfanya kuvaa nguo fupi katika kuigiza hata katika maisha yake ya kawaida.Elizabeth Kisiri dada Irene kama nitakua nimekukera nisamehe ivi kwanini huwa unapenda kuvaa nguo fupi mfano wa nguo ya klabu una akiwa unaigiza scene za ofisini?kwanini dada yangu wakati ofisini unatakiwa kuvaa suti au nguo yoyote ya heshima?
>>>>>>>Irene Uwoya nimezoea tu na napenda pia nguo fupi ndio maana siwezi kuvaa ndefu,maana nikivaa nguo ndefu nakereka,naweza kusema kuwa nina areji na nguo ndefu. MZEE MAJUTO NA JB KIBOKO Uwoya amesema kuwa katika kufanya kazi na wasaniii mbalimbali amekuwa akipenda sana kufanya kazi na mzee Majuto na Jb maana wanajua wanachokifanya katika kazi pia ndio watu ambao yeye amekuwa akiwapenda na kuwakubali katika tasnia ya filamu kwa Tanzania. Mudy Santos Ni msanii gan wa kiume anaependa kuigiza nae?
>>>>>Irene Uwoya Jb na Mzee Majuto SIJAWAHI KUJIUZA WALA KUIBA SIMU Moja ya shabiki alitaku kupata uthiobitisho kutoka kwa Irene kama alishawahi kufanya biashara ya mwili wake kama ambavyo amekuwa akisikia mtaani kuwa mkali huyo wa filamu kuna wakati alikuwa akijiuza na alishawahi kuhusishwa na wizi wa simu,na Irene alikana suala hilo na kusema hajawahi kufanya jambo kama hilo. Innocent Peter Eti ulikuwa unajiuza kwa laki 3 na uliwahi kuiba simu?Japo najua majibu yatakuwa hapana ila unieleze kiundani kidogo >>>>>>Irene Uwoya si kweliIrene Uwoya amekuwa kimya kwa muda mrefu katika tasnia ya filamu na amedai kwa sasa anajipanga na ujio wake mpya katika filamu na kuna filamu anafanya na rafiki yake wa karibu ambaye ni msanii na mchezaji pia Msamii baby.