Monday, June 15, 2015

UWEZO WA MAJANI YA PAPAI KATIKA TIBA

Papai ni moja ya tunda ambalo hupatikana kirahisi na ni moja ya tunda ambalo limekuwa likitumika kama tiba pia. 

Weekend hii nimeona ni vyema nikujuze hiza faida kadhaa za kutumia majani ya mpapai kama tiba. 

Kwanza kabisa juisi yake ya majanai ya mpapai husaidia kutibu vidonda, kinachofanyika ni kuweka juisi hiyo juu ya kidonda. Husaidia kupona.

Pia majani yake yanapokaushwa husaidia sana kutibu pumu, unachopaswa kufanya pale inapoanza kubana pumu utayachoma majani uliyoyakausha kisha jifukize utaona matokeo mazuri na kuachiwa kubanwa. 

Matumizi ya majani mabichi ya mpapai husaidia kwa wale wenye shinikizo la damu kwa kuyaloweeka katika maji ya mto na kunywa maji yake. 

Pamoja na hayo, kabla ya kutumia tiba hii ni vyema upate ushauri kutoka kwa wataalam wa dawa za mimea au mitishamba