Mchezaji huyo alifariki baada ya kupigwa risasi siku ya jumapili majira ya saa 2 usiku, Oktoba 26 akienda kumuokoa mpenzi wake aliyekuwa amevamiwa na majambazi nyumbani kwake, tayari mtuhumiwa wa kwanza amepandishwa kizimbani jana Oktoba 31.
Maelfu ya watu wamefurika uwanja wa Moses Mabhida, Durban mchana wa leo kwa ajili ya kuaga mwili wa golikipa huyo wakiwa wamevalia t-shirt zenye picha ya Meyiwa .