Monday, November 3, 2014

LULU:MAPENZI KITU GANI, NAHIFADHI NGUVU ZA KUJIFUNGUA

MASTAA wana mambo! Mtoto mzuri Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ametoa kali ya aina yake kwa kusema kamwe hatumii nguvu nyingi kwenye mapenzi kwa sababu yanapoteza muda bila sababu za msingi bora nguvu zake azitunze hadi pale atakapokuwa akijifungua.
Akimwaga cheche mbele ya mwanahabari wetu, Lulu alisema siku hizi wanaume wengi wanawafanya wasichana watumie nguvu kutetea penzi kutokana na migogoro isiyokuwa na msingi.
“Bora nguvu zangu nizihifadhi za kuendea leba kuliko kuzipoteza katika mapenzi kwani hayo mambo yamepitwa na wakati kabisa,” alisema Lulu.