Sunday, November 23, 2014

MAMA AWAPA KIPONDO NJEMBA 5 KISA WAME MTAPELI

ZAMANI kulikuwa na kasumba kwamba wanaume ndiyo huwapiga wanawake lakini hivi karibuni kibao kimegeuka ambapo mama mjasiriamali, aliyetajwa kwa jina moja la Mama Ashura ambaye ni mfanyabiashara wa viazi mviringo, anadaiwa kuwapa kipondo njemba watano kisa deni.
Mama Ashura akishusha kichapo hicho.
Kwa mujibu wa mashuhuda wetu, timbwili hilo ‘hevi’ lilijiri kwenye banda la chipsi la jamaa aliyetajwa kwa jina la Jerome Bertin Mushi almaarufu Babu lililopo jirani na Soko la Mji Mpya mjini hapa ambapo mwanamke huyo alifanikiwa kuondoka na beseni la kuku na chipsi. 
Baada ya zogo kuwa kubwa huku umati ukifurika eneo hilo, mmoja wa mashuhuda hao alimtonya mwanahabari wetu ambaye alifika fasta na kushuhudia mama huyo akipambana vilivyo na kundi la wanaume hao ambao aliwashinda nguvu kwa kuwashushia ngumi za kutosha.
...Akiondoka na beseni la chips.
Akihojiwa na mwanahabari wetu, mama huyo alifunguka huku akiangua kilio: “Babu alifika bandani kwangu wiki mbili zilizopita.“Alikopa gunia la viazi mviringo lenye thamani ya shilingi elfu sitini na moja, cha ajabu hadi leo hajanilipa fedha yangu.
“Kilichonifanya kuja hapa ni kwamba leo kaja sokoni kanunua gunia la viazi kwa mtu mwingine na akamlipa keshi hivyo nimeamua kumfuata anilipe deni langu.“Nimefika hapa anadai hana fedha, nimeamua kuchukua beseni lililojaa kuku na chipsi.”
...Akizidi kutokomea na beseni hilo.
Alipouliziwa kuku hao atawafanya nini wakati yeye siyo muuza chipsi, alijibu: “Hawa kuku ni wengi, najua nikikaa nao hadi kesho wataharibika, ikifika jioni kama hajaniletea fedha yangu naenda kuwatoa sadaka kwenye kituo cha watoto yatima na wazee wasiojiweza cha Funga-Funga.”
Kwa upande wa Babu alisema: “Nilipanga leo jioni nimlipe, cha ajabu kaja kufanya fujo ofisini, natafuta fedha nikamlipe maana kuku ni wa laki mbili na hili jua wataharibika.