Saturday, November 22, 2014

MAMBO YOTEE HADHARANI KIFO CHA BILIONEA

Stori: Hami da Hassan na Haruni Sanchawa
KIFO cha tajiri maarufu mjini Bukoba, Leonard Mtensa (50) ambacho kimetingisha kanda nzima ya ziwa, kilichotokea dakika chache baada ya marehemu kudaiwa kufanya mapenzi ndani ya gari lake, sasa mambo hadharani juu ya kila kitu kilichotokea, Risasi Jumamosi linakupa mkanda mzima.
Tajiri maarufu mjini Bukoba, Leonard Mtensa akichunguzwa na daktari.
Tukio hilo lililozua gumzo mjini Bukoba, lilitokea usiku Novemba 18, mwaka huu ambapo imeelezwa kuwa marehemu ambaye ni baba wa familia, kabla ya kupatwa na umauti, alikutwa ndani ya gari yake aina ya IST lenye namba za usajili T. 982 CQG akifanya mapenzi na mchepuko wake aliyetajwa kwa jina la Jackline Hassan (25) maeneo ya Buyekere mjini Bukoba.
Mwili wa marehemu, Leonard Mtensa ukitolewa hospitali ya mkoa wa Bukoba kupelekwa nyumbani kwake kuzikwa siku ya leo.
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini, siku ya tukio marehemu ambaye anamiliki Klabu ya Linas, alidaiwa kunywa pombe kali aina ya  Whisky Bond pasipo kula vizuri huku akisumbuliwa na tatizo la presha hivyo wakati akifanya yake ndani ya gari, ghafla presha ilipanda, akaanza kutapatapa.
Msafara wa magari ukitoka kuchukua mwili wa marehemu hospitali kuelekea nyumbani kwake.
“Si unajua tena jamaa umri umeenda kidogo na anasumbuliwa na presha, sasa inawezekana na kinywaji alichokunywa ndiyo kilitibua zaidi. Pombe ukiwa hujala huku una tatizo la presha madhara yake ndiyo haya,” kilisema chanzo chetu.
Mke wa marehemu akiwa haamini kama mumewe amefariki.
APEWA MSAADA
Baada ya hali yake kubadilika ghafla, inadaiwa kuwa mpenzi wake badala ya kukimbia kama ambavyo wengine hufanya, yeye alifanya juhudi kubwa kujaribu kuokoa jahazi kwa kupiga simu kwa marafiki wa marehemu, lakini kabla hawajafika, mtu mmoja alitokea na kumsaidia marehemu kumpeleka katika kituo cha Afya cha CLCT-Ndolage.
AFIA NJIANI
Chanzo hicho kilizidi kumwaga data kuwa, baada ya mtu huyo kujitolea kumkimbiza hospitali, hali ya Mtensa ilizidi kuwa mbaya ambapo alifariki kabla hajafika hospitali.
“Wakati wanamchukua kwenye gari, mapigo ya moyo yalikuwa yakimwenda mbio sana kabla hajafika hospitali akafariki,” kilisema chanzo chetu.
Binti aliyekuwa na marehemu.
HOFU KWA MREMBO
Chanzo kilidai kuwa, baadhi ya marafiki wa marehemu waliingiwa hofu na mrembo huyo na kuwa na wasiwasi wakihoji chinichini kwamba pengine alimpa marehemu kitu kibaya.
“Marafiki wa marehemu waliingiwa hofu sana na mazingira ya kifo, walikuwa wakijiuliza isije kuwa mrembo aliyekuwa naye amempa kitu chenye madhara,” kilisema chanzo chetu.
ASHIKILIWA NA POLISI
Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera, ACP Henry Mwaibambe alikiri kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema wanamshikilia Jackline kwa ajili ya upelelezi zaidi.
Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu.
AIBU, SIMANZI MSIBANI
Chanzo hicho kilizidi kueleza kuwa, msibani nyumbani kwa marehemu maeneo ya Kyakairabwa, kata ya Nyanga, waombolezaji walikuwa wakiona aibu kuzungumzia kifo chake hadharani kwa kuona ni kashfa hasa kwa kuwa marehemu alikuwa mtu anayeheshimika katika jamii.
Jeneza la marehemu, Leonard Mtensa.
“Unajua hakuna mtu hata mmoja ambaye anataka kuongelea kifo cha baba huyo, hata marafiki zake hawaongei kabisa kwani wanaona kuwa ni kashfa kwa sababu Mtensa alikuwa ni mtu maarufu sana si kwa hapa Bukoba tu, bali hata jijini Mwanza na kanda ya ziwa kwa jumla,” kilisema chanzo hicho.
WHISKY BOND IPOJE?
Ili kutaka kufahamu uhusiano wa kilevi alichokutwa nacho marehemu na kifo chake, Risasi Jumamosi lilimtafuta daktari mmoja mtaalamu wa magonjwa ya binadamu, (jina linahifadhiwa) ambaye alisema kitendo cha mwanaume kupoteza maisha akiwa anafanya mapenzi ni jambo la kawaida.
“Wako watu wanaofariki wakiwa wanafanya tendo, inategemea, wengine wanakuwa na historia ya magonjwa kama shinikizo la damu, sasa ile nguvu inayotumika katika tendo na kama ugonjwa utatokeza wakati huo, uwezekano wa kupoteza maisha ni mkubwa.
“Halafu pombe kama hii ni kali, sasa kama mtu alikuwa na matatizo ya presha, akawa amezidisha kiwango ni rahisi zaidi ku-collapse (hali kubadilika) wakati wa tendo. Tatizo lingine linaweza kuwa ni aina ya vyakula anavyokula kufuatia matumizi ya pombe yenye kilevi cha juu.
Mfano wa gari aina ya IST alipokutwa marehemu.
“Maana unakuta mtu mwingine anakunywa kilevi kikali lakini hapendi kula, hili nalo ni tatizo kubwa. Vinywaji vikali mara nyingi vinaendana na ulaji wa vyakula vyenye mafuta kwa sababu hivi huenda kukausha damu,” alisema.Marehemu aliyeacha mjane na watoto, alitarajiwa kuzikwa jana mjini humo.