“WANANIITA mshamba wa Kimanyema ila poa
tu!”Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Omary
Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, amesema baadhi ya
mashabiki wake wanamuita mshamba wa
Kimanyema, lakini hilo halimsumbui na wala
halimpi presha.
Nyota huyo anayetamba na wimbo
‘Ndagushima’, amesema hawezi kuacha
kufurahia kupiga picha nyingi iwezekanavyo
anavyosafiri nje ya nchi kwani ni kumbukumbu
kwake na pia ni kitu alichokiota kwa muda
mrefu.
“Eti wanasema mshamba wa Kimanyema
kapata vihela vyake eti kaenda shopingi,
nifanyaje sasa na ni kitu ninachokipenda,
sitaacha kutupia picha nikiwa nje au ndani ya
nchi kwa kuwa ni kitu ninachokipenda na
nadhani wengi wanapenda kwani ni sehemu
ya kufurahia maisha,” alisema Ommy Dimpoz.
Msanii huyo amekuwa katika ziara ya wiki
mbili sasa katika nchi mbalimbali ambapo
kesho Jumamosi, atatumbuiza katika Ukumbi
wa La Bodega huko Ufaransa baada ya shoo
iliyofanyika wiki iliyopita katika mji wa
Rotterdam, Uholanzi.