Saturday, November 1, 2014

PICHA 3 ZA KIVUKO CHA KWANZA NA KIPYA KILICHOTUA MTWARA OCTOBER 31.

2kvkHizi ni fursa ambazo kwa sasa wakazi wa Mtwara wanakutana nazo ambapo kwa kipindi cha nyuma hazikuwepo,hii imekuwa ni good news kwa wananchi wa Mtwara baada ya kupatiwa kivuko chao rasmi.
Mv Mafanikio ndiyo jina la kivuko hiki ambacho kitakuwa na kazi ya kuwavusha abiria na mali zao kutoka upande wa Mtwara Mjini kuelekea upande wa pili uitwao eneo la Msanga Mkuu.
Kivuko hiki kwa sasa kinasubiri kuzinduliwa kisha kianze safari zake,kimeingia leo Mtwara na wananchi kadhaa walijitokeza kukiangalia wakati kikijaribu kutembea kwenye maji.
Hiki ni kivuko cha kwanza ambapo kabla ya kivuko hiki kufika wananchi wengi walikua wakitumia mitumbwi kuvuka huku wenye magari wakizunguzuka bahari ili kuvuka na magari yao lakini kwa hiki kivuko magari na watu watavuka salama.

3kvk
1kvk