Monday, December 8, 2014

HIVI NDIVYO IDRIS ALIVYOJIZOLEA MILIONI 500 ZA BIG BROTHER AFRICA 2014

MSHIRIKI kutoka Tanzania, Idris Sultan usiku huu ameibuka mshindi wa shidano la Big Brother Hotshots na kujinyakulia dola za Kimarekani 300,000 zaidi ya milioni 500 za Kibongo.

Idris Sultan.
Idris ameshinda baada ya kuongoza kwa kura nyingi kutoka nchi tofauti.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Big Brother hivi punde, Idris amepata kura 5 akifuatiwa na Tayo kura 2, Macky2 kura 2, Nhlanhla naye kura 2, huku JJ, Sipe na Mam'bea wakijizolea kura 1 kila mmoja na Butterphly akiondoka bila kura yoyote.
Idris amepata kura kutoka nchi za Kenya, Namibia, Rwanda, Tanzania na Uganda. Tayo amepata kura za Nigeria na Msumbiji.
Macky2 amepata kura za Zambia na sehemu nyinginezo za Afrika huku Nhlanhla akiambulia kura za Afrika Kusini na Botswana.
Kwa ushindi wa leo, Idris amekuwa Mtanzania wa pili kushinda Big Brother Africa akiungana na Richard Bezuidenhout ambaye ni mshindi wa shindano la Big Brother Africa 2007.