Monday, December 8, 2014

KAULI YA AMANDA :" STAREHE KWANZA, MUNGU BAADAYE"

STAA mwenye shepu ya aina yake ndani ya Bongo Movies, Tamrina Poshi ‘Amanda’ ameibuka na kusema kuwa siku ikifika atarejea kwa Mwenyezi Mungu lakini kwa sasa bado anakula ujana.
 
Staa mwenye shepu ya aina yake ndani ya Bongo Movies, Tamrina Poshi ‘Amanda’.
Akipiga stori na Ijumaa Wikienda, Amanda alisema kwa sasa umri wake unamruhusu kula ujana kwa mambo ya starehe kama kuvaa mavazi ya kuacha mwili wake nusu utupu kwa sababu muda wa kurejea kwa Mungu bado haujafika. 
Amanda akipozi.
“Jamani niacheni na mavazi yangu, ukifika muda nitarejea naona mnanisema sana, kama wewe Mungu amekujalia kusali, mshukuru mimi muda huo bado haujafika,” alisema Amanda ambaye wakati huo alikuwa ametupia kivazi kilichomuacha wazi sehemu kubwa ya mwili wake hasa tumboni.