Thursday, December 11, 2014

MADAI YA MIMBA NJE YA NDOA, AUNT EZEKIEL AITWA BAKWATA

MADAI! Huku zikiwa zimepita siku chache tangu igundulike kwamba muigizaji, Aunt Ezekiel kuwa na mimba ambayo inasadikiwa kuwa si ya mume wake (Sunday Demonte), ndugu wa mume huyo wameibuka na kutaka kumfikisha Bakwata (Baraza Kuu la Waislamu Tanzania).
Muigizaji wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel (kulia) akiwa na shosti yake Wema Sepetu.
Ndugu hao ambao walizungumza na gazeti hili walidai kwamba wamesikitishwa na suala la muigizaji huyo kupata mimba huku akijua kwamba yeye ni mke wa mtu na ni kosa kubwa kwa mwanamke wa dini ya Kiislamu kupata mimba nje ya ndoa.
“Ni lazima tulisimamie kidete, haiwezekani mwanamke kaolewa halafu anapata mimba nje ya ndoa, hili suala tutalisimamia na lazima tumfikishe Bakwata,” alisema mmoja wa ndugu.
Alipotafutwa Aunt Ezekiel kulizungumzia hilo, alisema;
“Wanifikishe Bakwata kwa lipi? Kwani nimeolewa na ndugu au Demonte? Hawawezi kunifikisha Bakwata hivyo wasinifuatilie.”