Kwenye U Heard ya leo Decemba 01 2014 Gossip Cop Soudy Brown ameongea na mwigizaji Aunt Ezekiel kuhusu ishu mbili tofauti ambapo ya kwanza ni kuhusu rafiki yake Wema kama amewahi kumwambia chanzo cha kuachana na Diamond.
Ishu ya pili ni Diamond kuonekana na Zari kwenye Tuzo za Channel O Afrika Kusini siku ya Jumamosi, Aunt Ezekiel amesema hajui chochote kuhusiana na masuala hayo na kusema hawezi kuzungumzia masuala ya mtu binafsi.
Soudy Brown akamuuliza swali jingine ambalo linahusiana na namna alivyoonekana kama mjamzito kwenye show ya msanii Mirror siku ya jana Maisha Club ambalo pia Aunty amesema hana ujauzito ila ni gauni alilovaa linamuonyesha hivyo.
Nimekuwekea hapa U Heard, unaweza kuisikiliza kwa kubonyeza play hapa.