Jumapili ya Des 7 ni siku iliyochukua headline kwenye mitandao baada ya Davido kuwakwaza watanzania kwa kile alichokiandika kwenye twitter.Baada ya Mwakilishi kutokea Tanzania Idris Sultan kutangazwa kuwa mshindi wa Big Brother Africa Hotshots.
Mengi yamezungumzwa na watu,lakini leo Des 11 mshindi wa Big Brother Africa Hotshots,Idris Sultan alipata nafasi ya kuzungumza na vyombo vya habari mbalimbali miongoni mwa maswali aliyouliza ilikuwemo ile ishu ya Davido.
Mwandishi:Idris ukiwa kama mshindi wa BBA unazungumziaje ujumbe wa Davido uliowakwaza watumiaji wa mitandao?
Idris Sultan:Kwanza ningependa kusema nahisi ilikuwa ni utani kwasababu mwishoni mwa ile sentensi kumbuka kuna alama ya utani yaani ‘Lol’ sasa nimeshangashwa kuona watu wanaanza kuhisi vibaya kuwa ni dongo kwetu hapana.Ningewataka watanzania pamoja na Davido tusiingie kwenye migogoro isiyokuwa na msingi sisi sote ni bado vijana tunatakiwa kujitangaza na kupeana support hata vizazi vinavyokuja vijifunze vitu vizuri kutoka kwetu ikiwemo Upendo na Amani kati ya Tanzania na Nigeria’Alisema Idris Sultan.
Hizi ni baadhi ya picha kutoka kwenye mkutano huo