Monday, December 29, 2014

MKESHA WA KRISMASI, MKE WA MTITU AFANYA KIBAO KATA!

Mkurugenzi wa Kampuni ya 5Effects, William Mtitu akiwa na mkewe Yovitha Mtitu.

Mke wa Mkurugenzi wa Kampuni ya 5Effects, William Mtitu, Yovitha Mtitu, wikiendi iliyopita kwenye Mkesha wa Krismasi alifanya kibao kata nyumbani kwake ambapo alialika kikundi cha ngoma ya Baikoko na kukesha wakikata mauno na mastaa kibao wa Bongo.
Sherehe hiyo iliibua minong’ono kwani baadhi ya waalikwa walikuwa wakihoji sababu ya kufanyika kwa ngoma hiyo huku ukiwa ni mkesha wa sikukuu ya kidini ambayo wengi wao hukesha makanisani.
“Naona hela zinawasumbua hawa, hivi kwa nini wasipeleke kanisani wakatoe sadaka mbona wanapenda shughuli hivyo, kwa nini wanafanya kufukuru tena mkesha wa Krismasi?,” alihoji mwalikwa mmoja.
Mastaa waliofika kwenye shughuli hiyo ni Halima Yahya ‘Davina’, Shamsha Ford, Vanitha Omari, Sabrina Rupia ‘Cathy’, Eva wa Dude, Mke wa Cloud 112, mke wa Rado na wengine kibao.