Friday, December 26, 2014

SAFARI YA MABALOZI KUPANDA MLIMA KILIMANJARO KATIKA SIKU YA KWANZA

Desemba 16 mwaka huu Waziri wa Mambo ya nje ya Nchi ,Mh Benard Membe alikabidhi bendera kwa Balozi Adadi Rajabu kwa niaba ya Mabalozi ,ikiwa ni ishara ya kuanzisha safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro na safari hiyo ilianza kwa muda wa siku sita.
Baada ya kupumzika katika eneo la Kisambioni na kupata chakula ,safari iliendelea ya kwenda kituo cha Mandara.
Kila mmoja alikuwa na Morali ya juu wakati wote wa kupanda Mlima Kilimanjaro.
Baada ya kuongoza msafara wa Mabalozi kama ishara ya kuanzisha upandaji wa mlima Kilimanjaro kwa Mabalozi,hatimaye Waziri wa mambo ya nje ya nchi ,Mh Benard Membe alifika eneo la Nusu njia.