Friday, December 26, 2014

UFUKWE WA COCO BEACH DAR WAFURIKA WATU BURUDANI ZA X-MAS

Mwanamuziki Linex akikamua na kushangiliwa na mashabiki wake.
Umati wa watu ulifurika katika viwanja hivyo vya Coco Beach.Mmoja wa wasanii wa muziki akitoa burudani katika tamasha hilo.
Watoto wakiogelea baharini .
Farasi huyu alikuwa moja ya vivutio ufukweni hapo.
biashara zikiendelea beach.
biashara ya mataili ikiendelea.
MAMIA ya wakazi wa jijini Dar es Salaam jana walifurika katika ufukwe wa Coco Beach ili kupata burudani mbalimbali, hususani muziki,   kusherehekea Sikukuu ya Krismasi ambapo Kampuni ya Vodacom  ilifanya tamasha kubwa sehemu hiyo iliyovutia watu wa kila aina.