Imam wa Msikiti wa Kigogo Post uliopo Kigogo, Dar, Hemed Jalala, akizungumza na waandishi wa habari katika tukio hilo.Bango la kuwatakia Wakristo heri ya Krismasi na Mwaka Mpya kutoka kwa Waislam.Baadhi ya watu waliodhuhuria hafla hiyo wakimsikiliza Imam Jalala (hayupo pichani).Waandishi wa habari wakiwa kazini.
WAISLAM wa madhehebu ya Shia nchini wamewatumia Wakristo nchini salam za Krismasi na Mwaka Mpya katika moyo wa kupendana kiimani.
Ujumbe huo ulitumwa na Imam wa Msikiti wa Kigogo Post, jijini Dar es Salaam, Hemed Jalala, akisisitiza mshikamano na upendo kwa walimwengu wote bila kujali imani zao.