Thursday, December 11, 2014

TABORA; MSUSI WA SALUNI AFIA GESTI!

Kifo hakina huruma! Msusi wa saluni ya wanawake iitwayo HK iliyopo mjini hapa, aliyetambuliwa kwa jina moja la Ramadhan almaarufu Rama anadaiwa kufia katika nyumba ya kulala wageni (gesti) na kuibua utata mkubwa, kwani alikwenda kulala akiwa fiti kabisa hivyo polisi kupewa kazi ya kuchunguza kubaini kilichomuua.
Mwili wa Ramadhan ukipakizwa kwenye gari la polisi.
Kwa mujibu wa mashuhuda wetu, tukio hilo lilijiri wiki iliyopita kwenye Gesti ya Salama iliyopo Gongoni Manispaa ya Tabora mjini hapa ambapo lilikusanya umati kwa kuwa Rama alikuwa akifahamika kwa wengi.
Ilifahamika kwamba Rama aligundulika ‘amededi’ baada ya kutoamka hadi mchana.
Anayedaiwa kuwa mpenzi wake Ramadhan akiwa kwenye gari la polisi.
Ilisemekana kwamba baada ya kuona mazingira hayo ya kutatanisha, mhudumu aliita polisi ambao walifika na kuvunja mlango ndipo wakamkuta jamaa akiwa marehemu.
Kwa mujibu wa mhudumu huyo, ilikuwa ni siku ya tatu mfululizo kwa Rama kulala mahali hapo ambapo usiku wa tukio alifika na kupewa ufunguo wa chumba kama kawaida yake na wala hakuwa na dalili ya kuumwa.
Saloon iitwayo HK alipokuwa akifanyia kazi marehemu Ramadhan.
Ilisemekana kwamba baada ya polisi kufika eneo hilo, walivunja mlango wa chumba hicho na kuuchukua mwili wa Rama kisha wakaenda kuuhifadhi kwenye Hospitali ya Mkoa wa Tabora, Kitete kwa uchunguzi ambao bado unaendelea na kuwasaka ndugu kwa ajili ya mazishi.
Gesti iitwayo Salama ulipokutwa mwili wa marehemu Ramadhan.
Katika hali ya kusikitisha, alijitokeza mrembo aliyedaiwa kuwa ndiye mpenzi wake, ambaye alionekana mwenye huzuni na kwa muda wote alitoa ushirikiano wa kutosha kwa polisi ambao baadaye walimuachia.