MSANII wa muziki wa Kizazi Kipya Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amejikuta akikwaa skendo ya kuandika Kiingereza chenye makosa baada ya mtu asiyefahamika kufungua akaunti yenye jina la msanii huyo kwenye mtandao wa Facebook na kuandika ujumbe wenye makosa.
Maneno hayo ambayo yalikanushwa na Shilole, yalionesha kuwa msanii huyo anawaomba mashabiki wake wampigie kura msanii ambaye wanataka apafomu kwenye sherehe yake ya kuzaliwa kati ya Diamond Platnumz au BDK Yorobo.
“Hellow guys good morning on my birthday whitch guy can performance my birthday part please vote for me please vote for one who can join my part is Diamond Platnumz or BDK Yorobo…”
Baada ya maneno kusambaa mtandaoni yakiwa hayajanyooka vizuri na makosa ya kisarufi, wadau mbalimbali walimshambulia Shilole kwa maneno makali pasipo kujua aliyeandika si yeye.