Saturday, December 13, 2014

MUIGIZAJI ALIYESEMA "STAREHE KWANZA, MUNGU BAADAE" APATA AJALI!

MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Tamrina Poshi ‘Amanda’ amefunguka kuwa anamshukuru Mungu kwani amenusurika kifo kwa ajali ya bodaboda.Akizungumza na paparazi wetu, Amanda alisema ajali hiyo ilitokea hivi karibuni maeneo ya Makonde-Mbezi Beach jijini Dar wakati alipokuwa akiwahi lokesheni.
Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Tamrina Poshi ‘Amanda’.
“Nilirudisha gari nyumbani, nikachukua bodaboda ili iniwahishe lokesheni Posta, bodaboda alikuwa spidi likatokea lori la mchanga kwa mbele  katika jitihada za kulikwepa ndipo tukatumbukia mtaroni.
“Nashukuru Mungu nilipata majeraha madogo usoni, hakuna aliyeamini kama tumenusurika, nilienda Hospitali ya Masana na kupewa huduma ya kwanza, nikatoka,” alisema Amanda