Dunia na maajabu yake kwenye siku nyingine, leo kuna tafiti inayosema kuwa eti wanasayansi wanasema kwa kuangalia vigezo vya kibaiolojia wanaume wanaweza kunyonyesha hivyo huenda muda mfupi ujao jukumu hilo lisiwe la wanawake peke yao.
Dr. Semkuya kutoka Hospitali ya Mwananyamala amesema mwanaume anaweza kutoa maziwa lakini sio maziwa yafaayo kwa lishe ya mtoto.
“… Wapo wanaume wanaochezea chuchu kwa muda mrefu na kufanya hivi wanaweza kusababisha maziwa kutoka…”—Dk. Semkuya
Daktari mwingine mstaafu anasema hivi; “Wanaume wana tezi zao na wanawake wana tezi za kipekee ambazo zinawasaidia kuzalisha maziwa…”— Dk. Malise Kaisi.
Daktari mwingine bingwa wa magonjwa ya binadamu Meshack Shimwela amesema mwanaume anaweza kutoa majimaji katika chuchu zake lakini hayo sio maziwa.
Iliwahi kuripotiwa kuwa mwaka 2002 kulikuwa na mwanaume aliyeamua kumnyonyesha mwanae baada ya kufiwa na mke wake Sri Lanka, lakini story ni kwamba Jarida laLancet limeeleza kuwa mwanaume anapokaa na mtoto mchanga na kuamua kunyonyesha tezi za maziwa zinazoitwa lobules huzalisha maziwa hivyo kukawezekana mwanaume kunyonyesha maziwa kama ya mwanamke.
Ripoti ya Jarida hilo imesema kwa watu wenye jinsia mbili kuna uwezekano sio wa kunyonyesha tu, bali hata kubeba ujauzito kutokana na mchanganyiko wa homoni.
Comment yako mtu wangu wa nguvu, unadhani ikithibitika hii ya wanaume kunyonyesha hali itakuwaje?
Chanzo cha Habari: Gazeti Mwananchi, December 26.