Mitandao ya kijamii na vyombo mbalimbali vya Habari leo viliripoti kuhusu mtu mmoja raia wa Sierra Leone, Abdul Koroma ambaye alikuwa anashikiliwa na Jeshi la Magereza nchini kufariki dunia leo Dar baada ya kupigwa risasi na askari Magereza wakati akijaribu kutoroka.
Mtu huyo alifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa mara ya kwanza mwaka 2013 kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya na kushitakiwa.
Ameuawa katika uzio wa Mahakama hiyo baada ya kumtoroka askari magereza aliyekuwa amemsindikiza kujisaidia ambapo alijaribu kuruka ukuta wa mahakama hiyo.
Shuhuda mmoja wa tukio hilo amesema; “alikimbilia kwenye ule ukuta pale, akapandisha mpaka pale juu… anataka arukie upande wa pili magereza washatokea, wakaona hawawezi kukimbia yuko mbali ndio wakampiga zile risasi kama tatu hivi ndio akafariki…”
Akizungumzia tukio hilo Msimamizi wa Mashtaka Mahakama ya Kisutu Tumaini Kweka amesema; “Wakati wapo kwenye sero ndipo yeye akajaribu kutoroka kwa kujaribu kuruka ule ukuta wetu wa Mahakama ndipo wanausalama wetu ambao wako hapa wakaweza kundhibiti…“
Kuwasikiliza shuhuda wa tukio hilo na msimamizi huyo wa mashtaka sauti iko hapa.