Friday, January 2, 2015

AMANDA: 2014 ULIKUWA FULL MAJANGA KWANGU

Msanii wa filamu Bongo, Tamrina Posh ‘Amanda’ amesema mwaka uliopita wa 2014 ulikuwa mbaya sana kwake kwani aliandamwa na majanga yaliyotikisa maisha yake.
Msanii wa filamu Bongo, Tamrina Posh ‘Amanda’.
Akizungumzia namna alivyoupkea mwaka wa 2015 Amanda alisema, kwanza anamshukuru Mungu kwa kuuona akiwa mzima lakini akamuomba amuepushe na mabalaa kwani uliopita haukuwa rafiki kwake.
“Mwaka 2014 bora umeisha, ulikuwa mbaya sana kwangu, mwanzo ulikuja vizuri lakini nikashangaa katikati ukanigeuka, nimenusurika kifo lakini namshukuru Mungu naendelea kupumua hadi leo,” alisema Amanda.