WAPIGANAJI wa Taifa la Kiislam (ISIS) lililoanzishwa katika maeneo ya Syria na Iraq, wametoa picha za maofisa wanane wa polisi wa Iraq waliokamatwa na kuuawa kwa kufanya ujasusi dhidi ya ISIS kwa ajili ya serikali ya Iraq.
Kwa mujibu wa habari kutoka Taifa la Kiislam, kiongozi wa watu hao alitajwa kama Kepteni Hossam Salah Bnosh ambapo yeye na wenzake walibadili madhehebu yao na kujiunga na madhehebu ya Kiislam ya Sunni, lakini baadaye wakachukua fursa hiyo kufanya ujasusi dhidi ya ISIS.
Mauaji hayo ambayo yalifanyika mchana, yalikuwa na lengo la kuwaonyesha walimwengu adhabu hiyo iliyotolewa kwa watu hao ambao walikuwa wamevishwa ‘magwanda’ ya rangi ya chungwa kama wavaayo wafungwa wa gereza la Guantano linalomilikiwa na Marekani huko Cuba.