LICHA ya kushauriwa na daktari kuhusu kutulia na kutovaa viatu virefu kutokana na ujauzito, mwigizaji Aunt Ezekiel ameonekana kuwa ni sikio la kufa kwani ameendelea kuvaa kama kawaida.Aunt aliendeleza ubishi huo Jumatano iliyopita mjini Dodoma alipokuwa amekwenda katika Pati ya Good Bye 2014 iliyoandaliwa na Kampuni ya Endless Fame ambapo mashabiki walimshuhudia Aunt akiwa amevaa kigauni kifupi pamoja na viatu virefu kama kawa.
Mwigizaji wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel.
“Mh! Huyu Aunt si kashauriwa apumzike maana tumbo kubwa na asivae viatu virefu, mbona anaendelea sasa?,” alihoji shabiki mmoja.
Hivi karibuni Aunt alishauriwa na daktari mmoja wa Dar aitwaye Chale kutovaa viatu virefu kwani huweza kumsababishia matatizo mtoto aliye tumboni.