Monday, January 5, 2015

AY AKANUSHA KUWA NA MAHUSIANO NA SITTI MTEMVU NA VICTORIA KIMANI, ASEMA KWA SASA YUKO SINGLE

Miongoni mwa watu maarufu wa Bongo ambao huwa hawapendi kuweka hadharani mahusiano yao ya kimapenzi ni pamoja na Ambwene Yessaya a.k.a AY. Baada ya kumuweka hadharani mchumba mpenzi wake 2013, AY amesema kwa sasa yupo single tena.
AY na mchumba 2
AY na aliyekuwa mchumba mwenye mchanganyiko wa Yemeni na Shelisheli, kwenye Red Carpet ya Road to CHOAMVA 2013, Club Billicanas
Hilo limefahamika baada ya kubananishwa na paparazi aliyemuuliza kama ni kweli ameanzisha uhusiano wa kimapenzi na aliyekuwa Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu ambaye weekend iliyopita alikuwa miongoni mwa watu aliowaalika kisiwani Mbudya kula bata, AY alikanusha taarifa hizo.
Sitti3
Sitti Mtemvu
“Pale umekaa au umepita? Aliulizwa (akimaanisha kwa Sitti), na jibu lake lilikuwa “Aah wapi wewe, ntaanzaje kwanza,
kukaa kwa mtu si unakaa tu ukitaka, ukitaka mtu unakaa na unaweza kuwaambia watu umekaa sehemu flani”.
vicy
Victoria Kimani
Katika swali lingine aliulizwa kama ana uhusiano na msanii wa Kenya. “Hivi AY wewe girlfriend wako yule kabisa kabisa ni Victoria Kimani eeh?” Na jibu lake lilikuwa “sina…sina mtu sina mtu” 
Jibu hilo linamaanisha kuwa staa huyo hayuko tena na yule aliyekuwa mchumba wake mwenye asili ya Yemeni na Shelisheli.
Single Ladies, mzee wa commericial ndo kashaweka wazi status yake ya sasa kuwa yupo single